Dr Ali Mohmed Sheni amewakemea wanoutaka uongozi kwa kutumia misikiti Unguja.
Dr Shein ametioa kauli hiyo huko Makunduchi wilaya ya kusini Unguja
wakati akiongea na waumini wa kiislamu baada ya kuuzindua na kuufungua
msikiti mpya uliojengwa kwa nguvu za wananchi na kushirikaina na
wafadhili ambapo amesema msikiti ni nyumba ya ibada nasio mahali pa
kutafuta umaarufu au uongozi na sehemu hiyo iheshemiwe nasiyo mahali pa
mivutano na migogoro.
Mbali yakuufungua msikiti Alhaj Dr Shein baadaye alapata fursa ya
kufungua madrasaa ya kisasa iliyojengwa huko kiungoni ambayo inatarajiwa
kutoa elimu ya dini na kijamii kwa watoto wa Makunduchi ambapo
aliwataka wazeee kuwa karibu na vijana wao nasio kuwachiasuala la elimu
kwa waalimu pekee kwa vile watoto hao ni tegemeo kubwa la baadaye, kwa
upande wake waziri wa kazi na utumishi wa umma ambaye pia ni mwaklishi
wa jimbo hilo Mhe Haroun Ali Suleiman amesema ujenzi wa msikiti na
madrasaa umewezekana kutoakana na umoja wa wananchi walionyesha kwa
wafadhili.
Msikiti huo ambao upo tokea miaka zaidi ya miaka 100 na ujenzi wa
madrassa huku ikiwa ni harakati za uongozi wa jimbo hilo kuhakiksiha
vijana wanpata elimu wakiwa karibu na maeneo ya makaazi badala ya
kuhangaika na kutembea maneo ya mbali.








0 comments: