Wafugaji waiomba serikali kuangalia namna ya kuweza kudhibiti wahalifu na wahamiaji haramu loliond
Wananchin hao wamemweleza mkuu wa mkoa wa arusha Bw.Felexs
Ntebenda kijiko aliyetmbelea eneo hilo kuwa pamoja na kuwepo kwa
ushirikiano mzuri na wenzao wa nchi jirani hasa wakati matatizo
yakiwemo ya kiangazi baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya fursa
hiyo ikiwa ni pamoja na kugoma kurudi makwao.
Wazee wa mila wa kabila hilo wamesema hadi sasa hakuna tatizo
lolote kwani wanaendelea kudumisha amani kwa kutumia viongozi wao wa
mila wenyeviti wa mitaa na mabalozi wa nyumba kumi lakini hali
inavyokwenda wanahitaji msaada wa vyombo vya dola.
Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa mkoa Bw.Ntebenda amesema serikali
itajenga kituo kikubwa cha polisi na ofisi ya uhamiaji katika eneo hilo
ili sheria ziweze kufuatwa.








0 comments: