Wafugaji Tunduru wamuomba rais Magufuli kukomesha migogoro ya wafugaji na wakulima.



Wafugaji wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamemuomba rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli kukomesha migogoro ya wafugaji na wakulima nchini ambayo imepoteza maisha ya wafugaji na wakulima na pia wamemuomba kuweka uasawa  baina ya wananchi na wawekezaji.
Wametoa ombi hilo katika kijiji cha Kidodoma wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakati wakizungumza na ITV ambapo wafugaji wilayani humo wana Ngo’ombe zaidi ya thelasini na nane  elfu ambazo walihama nazo toka bonde la ihefu mkoani mbeya.
 
Licha ya kumpongeza Dkt John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rais wa tano wa Tanzania lakini wamemuomba kuwatambua wafugaji kwa kuwa wamekuwa wakichangia pato serikalini kupitia mifugo yao lakini hawathaminiwi na mifugo yao inaonekana ni haramu.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Kidodoma wilayani Tunduru Bw. Alifa Msusa Makunganya amesema wamekuwa na mahusiano mazuri na wafugaji hao na wamekuwa wakichangia pesa katika maendeleo ya kijiji.

0 comments: