Polisi Tanga wamefanikiwa kukamata Shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi.


Jeshi la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kukamata shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 462 iliyokuwa imehifadhiwa katika magunia aina ya viroba ikitokea Arusha kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusambazwa kwa mawakala kwa ajili ya kuuzwa kwa watumiaji.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga kamishna msaidizi wa Polisi Zubeir Mwombeji amesema katika tukio hilo jeshi la Polisi limewatia mbaroni watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na shehena ya hiyo ya mirungi na kuwataja kwa majina kuwa ni dereva wa gari aina ya fuso lililokuwa limehifadhi mirungi na Aloyce Gabriel mkazi wa picha ya ndege Kibaha na Rashid Juma mkazi wa Mbauda mkoani Arusha.
 
Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wakielezea hatua hiyo wamesema ili kudhibiti usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi ni vyema askari wa jeshi hilo wakaimarisha doria sehemu za mipakani ambapo wafanyabishara kutoka nchi jirani ya Kenya kwa kushirikiana na wenzao waliopo katika vijiji vilivopo pembeni mwa bahari ya Hindi mkoani Tanga wamekuwa wakipitisha bidhaa hiyo haramu kwa njia za panya pasipo kukamatwa.
 
Kufuatia hatua hiyo kamanda Mwombeji amewataka wafanyabiashara wenye magari ya mizigo na abiria kuachana na bishara ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kwa sababu jehsi la polisi litataifisha chombo cha usafiri kilichohusika na usafirishaji wa bidhaa hiyo haramu kisha watuhumiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

0 comments: