SITTA awaasa Urambo
WAZIRI wa Uchukuzi SAMWEL SITTA amewaasa wananchi wa wilaya ya URAMBO mkoani TABORA kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili waweze kuipigia kura katiba inayopendekezwa april 30 mwaka huu.
SITTA ambaye ni Mbunge wa URAMBO amesema vitambulisho hivyo vitawawezesha kupigia kura ya maoni Katiba inayopendekezwa na vitatumika pia katika uchuguzi mkuu wa madiwani, Wabunge na Rais.
Akizungumza na Wananchi wa mji wa URAMBO, mkoani TABORA Waziri wa Uchukuzi SAMWEL SITTA amewataka wananchi wenye umri wa kuanzia miaka 18 wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura pindi zoezi hilo litakapofika wilayani URAMBO.









0 comments: